GET /api/v0.1/hansard/entries/624480/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 624480,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624480/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Spika, utakumbuka kwamba humu nchini kulikuwa na viwanda vya makonge, bixa, korosho na nyama, miongoni mwa viwanda vingine, ambavyo hivi sasa haviko. Kwani nchi yetu ina nini? Aidha tunaanzisha viwanda tukiwa na nia ya kuvipora baadaye ama utendakazi wetu ni hafifu. Wakati umefika wa kujiuliza: “Jamani, tunaenda wapi Wakenya, na ni kitu gani tunachohitaji kufanya ili tuiboreshe hali hii?”"
}