GET /api/v0.1/hansard/entries/624481/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 624481,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624481/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Katika sehemu ya magharibi ya nchi, wananchi wengi wanategemea sukari katika maisha yao ya kila siku. Wakulima hupanda miwa ambayo wanaitegemea kuwaelimisha watoto wao na kupata ajira zinazowawezesha kulea familia zao. Ni kitu gani kimetokea hivi sasa? Hivi sasa, watu wamefadhaika na kukata tamaa. Hawana mbele wala nyuma kwa sababu ya mambo ambayo tumeyaona kwenye Ripoti hii. Ripoti hii imeeleza kwamba kuna ufisadi wa hali ya juu katika sekta ya sukari humu nchini. Kuna masuala ambayo hayajatekelezwa vizuri. Mara nyingi Serikali huleta kampuni kutoka nje kusimamia utendakazi katika viwanda vyetu vya sukari lakini punde wasimamizi wa kampuni hizo wanapowasili humu huangalia na kuona kwamba kuna nafasi ya kujitengenezea fedha. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}