GET /api/v0.1/hansard/entries/624512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 624512,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624512/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Mhe. Spika, ni vyema kuona kamati tekelezi ikifuatilia suala hili na kuhakikisha kwamba Ripoti hii imetekelezwa kikamilifu na kwa wakati unaofaa. Tumeona kamati nyingi zikiwasilisha Ripoti zao Bungeni lakini Kamati Tekelezi haifuatilii na kuhakikisha kwamba ripoti hizo zinatekelezwa vilivyo. Tunajiuliza ni kwa nini viwanda vya sukari vinaanguka nchini Kenya? Hatuzungumzii kiwanda cha sukari cha Mumias peke yake bali tunazungumzia kiwanda cha sukari cha Ramisi, na kiwanda cha nyama cha KMC kule Mombasa, ambacho kiko katika constituency yangu. Tunasikitika kwamba viwanda hivi vinaendelea kuanguka badala ya kuimarika. Vinatusababishia matatizo makubwa. Bidhaa hii adimu, ambayo watu wanataka kuitumia, haitatumika kwa sababu kuna shida katika viwanda hivi. Pia, maafisa wa KRA ni lazima wawe waadilifu na wafanye kazi yao vizuri. Tunaona bidhaa zikiingizwa nchini bila kulipiwa ushuru. Hatimaye watu wanaagiza bidhaa kutoka nchi za nje na kususia kuvikuza viwanda vyetu. Kwa hivyo, ninayaunga mkono yote yaliyopendekezwa kwenye Ripoti hii ili wale wote ambao walifanya uhalifu, na wahusika kwenye mambo yote mabaya, wachukuliwe hatua za kisheria na kuadhibiwa. Mhe. Spika, kwa hayo machache, ninaiunga mkono Ripoti hii."
}