GET /api/v0.1/hansard/entries/624588/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 624588,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624588/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kama nilivyosema, ugatuzi umetusaidia sana katika nchi yetu ya Kenya lakini ufisadi bado umekithiri katika sehemu nyingi. Ni lazima tulishughulikie jambo hili vilivyo kama Serikali ili tuwe na maadili mema ya kujimiliki katika nchi hii. Pia, bado hakuna usawa wa kijamii katika kumiliki afisi nyingi sana katika nchi hii. Kuna kelele nyingi sana kutoka kwa jamii nyingi ambazo ni dogo. Kwa mfano, jamii yangu ya Wajomvu ni dogo sana katika nchi hii lakini inatambulika katika makabila ambayo yako hapa nchini. Bado makabila madogo kama haya hayajazingatiwa vilivyo. Pia, ningependa kuunga mkono mwenzangu, Mhe. Ochieng. Amezungumza kuhusu usawa katika kugawanya kazi katika miradi mikubwa ya nchi. Tukiangalia kama vile mradi mkubwa wa Standard Gauge Railway, ambao unafanyika pale kwangu Miritini, vijana wengi sana bado wanalia kwamba hakujakuwa na usawa wa faida kutoka kwa mradi huu. Ni muhimu tujizatiti na kufanya usawa huu ili vijana wetu wafaidike katika maadili mazuri na tuishi na mipango mizuri ambayo inawekwa na Serikali. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninakushukuru kwa kunipatia fursa hii kuchangia. Kama nilivyoahidi nitachangia kwa dakika mbili, sikuongeza hata moja."
}