GET /api/v0.1/hansard/entries/624667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 624667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624667/?format=api",
"text_counter": 354,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii tena kuchangia Ripoti hii. Kusema kweli, katika nchi yetu ya Kenya, kuna mambo mengi ambayo tumefanya ya kimataifa, jambo moja likiwa ni lile Kongamano la Biashara ambalo lilifanyika katika ukumbi wetu wa Kenyatta International Conference Centre (KICC), Nairobi. Pia, ni muhimu sana kuona kuwa katika yale mambo ya kimataifa ambayo tunajihusisha nayo, tunapaswa tuhusike sana kama vile ndugu yetu, Mhe. Katoo, ameeleze kuhusu mambo ya Afrika Mashariki. Tunafaa kuangalia yale ambayo yanaendelea katika Afrika Mashariki. Tukiwa nchi ambayo imekomaa, tunaona kuwa kuna shida nchini Burundi na tunafaa kujiuliza nchi yetu inafanya nini katika mambo ya Afrika Mashariki ili watu wasiwe na matatizo na tuweze kuishi sote kama kitu kimoja. Vilevile, katika nchi tofauti ambazo tumeenda kama Kamati, tunaleta mengi kama Ripoti ambazo tunaandika. Ni muhimu sana kama nchi kuiga yale ambayo ni ya manufaa ili tuweze kuendelea mbele kama vile nchi nyingine. Ninasema hivi kwa sababu juzi, Kamati ya Uwiano na Mshikamamo wa Kitaifa, ambayo mimi ni Mwanakamati, tulikuwa Abuja, Nigeria. Jambo kubwa ambalo tulisoma pale ni kuwa kuna hali za kuthibiti matatizo ya mwanzo mwanzo ambayo kwa Kiingereza yanaitwa early warning signs . Wamezitumia sana katika muungano wa Economic Community of West African States (ECOWAS) kuthibiti mambo mengi ya kupigana na kama vile Boko Haram na mambo mengine zaidi. Sisi pia tuna matatizo kama haya ya AlShabaab katika nchi yetu ijapokuwa katika Ripoti ya Rais, ambayo imepita ambayo ningependa sana kuchangia, ametuonyesha vile ambavyo nchi yetu inaweza kuthibiti matatizo haya ya usalama. Kwa hivyo, kama tungeweza kuyaiga hayo, ingekuwa vizuri sana. Tukifanya jinsi ECOWAS inavyofanya, sisi pia, kama Jumuia ya Afrika Mashariki na Kati, tutaweza kuishi kwa njia ya kisasa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}