GET /api/v0.1/hansard/entries/624914/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 624914,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/624914/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa fursa hii. Kwanza kabisa, ninasimama kuiunga mkono Hoja hii. Pili, Kenya ilipopata Uhuru, kulikuwa na SessionalPaper No.2 . Sera hii iligawanya Kenya katika sehemu mbili; sehemu ya rotuba na sehemu isiyokuwa na rotuba. Huduma katika taifa imegawanywa kwa msingi wa sera hii. Wakenya wengine wanapozungumza kuhusu utoaji wa kitambulisho, mimi nahisi kulia. Kule kwangu, utapata mama amezaa watoto watano na mpaka leo hana kitambulisho na hawezi kutembea barabarani kwa sababu Kenya Defence Forces (KDF) wako katika kila kona. Kitu cha kwanza watamuuliza ni atoe kitambulisho na si makosa ya yule mama kutokuwa na kitambulisho. Lakini wale wanaowasajili Wakenya, kwa furaha yao au uwezo wao, wanakufanya Mkenya au usiwe Mkenya. Wamemnyima yule mama fursa ya kupata kitambulisho. Swala la pili ni muda ambao unahusika katika utoaji wa kitambulisho. Kuna mtu ambaye amebeba kadi ya kusubiri kwa miaka mitatu au minne. Masuala ya utoaji wa vitambulisho ni masuala ya dhuluma dhidi ya binadamu. Unamnyima mtu haki yake ya kuwa Mkenya. Unaambiwa kuwa Cheti cha Kuzaliwa hakithibitishi uraia wako. Kitambulisho na hati ya kusafiria ndizo zinathibitisha uraia wako. Huwezi kupata hati ya kusafiria kama huna kitambulisho. Wakati umefika wa kuwanasua Wakenya kutoka kwa dhuluma ya Sessional Paper No.2 na kutoa uhuru wa kila Mkenya kumiliki kitambulisho. Kwa sababu, uraia wako, rasilimali yako na biashara yako haziwezi kuwepo kama huna kitambulisho. Kuweka usalama ni jukumu la Serikali ya kitaifa lakini kaunti zinafanya kazi nzuri. Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ni jukumu la Serikali ya kitaifa lakini kaunti zinafanya kazi nzuri. Kwa nini vitambulisho visitolewe katika kaunti? Ile huduma itakuwa rahisi kwa Wakenya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}