GET /api/v0.1/hansard/entries/625094/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 625094,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/625094/?format=api",
"text_counter": 412,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "kabisa inaambatana na Katiba yetu kuhusu ugatuzi. Sisi ambao tuko karibu na mpaka tuna matatizo mengi sana wakati tunatafuta vitambulisho lakini tukipitisha Hoja hii, haya matatizo yatapungua. Imekuja wakati mwafaka, mzuri na sawa sawa kabisa. Ningependelea, ikiwezekana tuweke marekebisho mengine maanake mtoto anapozaliwa anapata cheti cha kuzaliwa na vile vile wakati huo huo akitafutiwa pasi ya kusafiri nje inapatikana. Ingewezekana pia kitambulisho kingepatikana wakati huo huo. Vile vile, kuna Cheti cha Tabia Nzuri kutoka kwa maafisa wa usalama kinachoitwa kwa Kiingereza, Certificateof Good Conduct ambacho pia kinasumbua sana vijana. Tungesaidika sana ikiwa vyeti hivi vingeshikanishwa vyote kwa pamoja. Pia kuna nambari inayotumika katika National Treasury inayoitwa Integrated Financial Management Information System (IFMIS). Sioni sababu gani vitambulisho visigatuliwe. Vikigatuliwa, wananchi wengi wataweza kupata vitambulisho. Kwa sasa hivi, kuna wazee, kina mama na waume ambao wako zaidi ya umri wa miaka 50 ambao bado hawana vitambulisho kwa sababu ni gharama kubwa kwenda kila saa kwa afisi kuulizia kuhusu hivyo vitambulisho. Wale maafisa hawako kule mashinani. Vitambulisho hivyo vikishapelekwa pale afisini Nairobi, kufuatilia inakuwa vigumu kwa sababu hujui ni wakati gani vinatoka. Lakini vikigatuliwa, kulingana na Hoja hii, Wakenya watasaidika kwa kupunguza gharama, muda na zile nguvu ambazo mtu anatumia kuvitafuta vyeti hivi. Wenzangu wameongea mengi. Naunga mkono Hoja hii na hayo marekebisho ambayo yamefanyiwa na Mheshimiwa sasa hivi."
}