GET /api/v0.1/hansard/entries/625885/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 625885,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/625885/?format=api",
    "text_counter": 539,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "hazijakamilishwa zimekamilishwa na vipande vya ardhi ambavyo vina utata vimeratibiwa. Zaidi ya hivyo, tunafaa kuhakikisha kuwa majukumu ya Jopo hili yametimizwa kabla muda wao haujaisha. Nashukuru Kamati ya Ardhi kwa kuondoa yale mapendekezo ambayo walikuwa nayo ya kubadilisha fedha ambazo zilikuwa zimepatiwa kitengo hiki kwa sababu imebainika wazi kuwa mara nyingi, kitengo hiki kinanyimwa fedha ndio maana kinashindwa kutekeleza wajibu wake. Vile Mhe. Amina amesema alivyokuwa akichangia, naomba nimuunge mkono kwa dhati alivyosema kuwa katika nchi hii ya Kenya, madini yameanza kuleta faida na kuchangia katika kuzalisha fedha ambazo zinahitajika nchini. Lakini ni vizuri tuangalie fedha ambazo Wizara zinazohusika na madini zinapewa. Wakati mwingine waliomba shilingi bilioni nne na wakapewa chini ya bilioni moja. Wakati huu, tunaomba angalau wapewe bilioni mbili lakini pia hilo linaleta shida. Wakati umefika nchi hii ijue rasilimali yake ambayo iko chini ya ardhi. Ukiuliza Mkenya kiasi cha madini ambacho kipo chini ya ardhi, hawezi kusema kwa sababu vifaa ambavyo vinahitajika kutupatia utaratibu wa kujua kiasi cha mali chini ya ardhi havijanunuliwa. Nchi hii inaelekea wapi? Iwapo tunajua tuna rasilimali na madini, kwa nini tungojee watu watoke nje, waje na vifaa vyao na kupima na kujua kiasi cha madini chini ya ardhi na waanze kuyachimbua wakati nchi imenyamaza? Wakati umefika tuhakikishe kuwa vitengo ambavyo vinaweza kuzalisha fedha nchi hii vimepewa pesa ya kutosha. Madini yapatiwe vifaa ambavyo vinafaa kupewa watu ambao wanavihitaji na upimaji uwe ni wa kutosha. Kila mtu ambaye anataka kuingia katika sekta hii ya madini apewe nafasi ili kutoa mchango wake wa kuzalisha mali. Ningependa kuongea kuhusu suala la maji. Kama tunavyojua, wakati wa ugatuzi, sekta ya maji imegatuliwa lakini tuna Wizara ya Maji. Vile tujuavyo, katika Bunge la Kumi, tulichukua mkopo kutoka China wa kutengeneza bomba la pili kutoka Mzima kuenda Mombasa. Nini imefanyika na hizo fedha? Wenzangu ambao tulikuwa nao katika Bunge la Kumi tukipitisha huo mkopo, na sote tulikuwa hapa wakati huo, Waziri alikuwa Mhe. Charity Ngilu. Alikuja hapa akatueleza wazi wazi kuwa fedha hizo za kwanza zingetumiwa kurekebisha bomba na katika awamu ya pili ya kuleta bomba la pili kutoka Mzima kwenda Mombasa watu wa Taita ambao wako hapo katikati wawe na maji ya kutosha. Watu wa Voi, Mbololo, Kishushe na Mwakitau wawe na maji ya kutosha. Nini kimetokea? Fedha hizo zijui nazo pia zimeingia katika lile kapu ambalo tunalijua siku hizi la kuingia lakini kutoka ni shida."
}