GET /api/v0.1/hansard/entries/625887/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 625887,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/625887/?format=api",
    "text_counter": 541,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Jambo lingine ambalo ningependa kuangazia ambalo limezungumziwa na wenzangu ni kuhusu fedha za wazee. Wazee wamelalamika. Tunasema tunaongeza hizi fedha lakini nikiangalia hapa, hazijaongezwa. Zimebanwa. Tunasema kuwa zitakuja kuongezwa mwaka mwingine. Ni nini kimetokea na hawa wazee wetu bado nao wamejitoa mhanga kuhakikisha kuwa taifa linakuwa? Wamejibidiisha vile wawezavyo kushikilia taifa lakini tukifika wakati wa kuhakikisha wamepata kitu angalau kabla maisha yao hayajafika kikomo, tunawanyima fedha."
}