GET /api/v0.1/hansard/entries/625941/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 625941,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/625941/?format=api",
    "text_counter": 595,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa muda huu ambao umenitunukia niweze kutoa mchango wangu kuhusu Mswada huu wa Ardhi ya Wenyeji . Kama tunavyojua wenyeji ni watu ambao wamekuwa mahali tangu miaka iliyopita na ardhi ambayo wanaikalia kulingana na vitengo vya sheria ni yao. Shida iliyopo ni kuwa mpaka sasa tangu tupate Uhuru, ardhi hiyo imechukuliwa kiholela. Mtu yeyote ako huru kwenda kuikalia vile anayvotaka. Mapendekezo ya sheria hii inasema kuwa sheria hii ikipitishwa, ile ardhi ya wenyeji, wale watu wameenda wakakaa pahali hapo, wakijikusanya wawe kama kitengo kimoja, wanaweza kupatiwa hiyo ardhi iwe yao. Wakati umefika watu waheshimiane na pia wakati umefika watu wasiwe wanafurukushana kwa ardhi kiholela. Hii ni kwa sababu kuna watu wamekaa kwa hiyo ardhi miaka nenda miaka rudi. Leo hii ukimwambia unamwondoa, ataenda wapi? Pale alipokaa kunabainika pale ni kwake. Hata hivyo, kuna sehemu nyingi hapa nchini ambazo ardhi za wenyewe zinatumika kiholela. Naomba nitoe mfano. Hivi sasa kuna upimaji wa mashamba unaendelea huko Taita Taveta sehemu za Njukini. Kuna ardhi inagawanya. Mpaka leo hatujaambiwa ni ardhi ya nani. Tunaambiwa ni ardhi imetolewa kwa familia, eka 2,000. Imetolewa na nani? Katika vikao vyetu, katika Kamati ya Ardhi tumeomba tupatiwe orodha ya watu wote ambao wanatarajiwa kuhifadhiwa kwa hiyo ardhi. Ni akina nani? Ni wenyeji? Wametoka wapi? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}