GET /api/v0.1/hansard/entries/625942/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 625942,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/625942/?format=api",
"text_counter": 596,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ama la sivyo ardhi kama hizi zinaweza kutumika vibaya hasa wakati huu wa kisiasa. Watu watoke sehemu zingine waje wapewe vipande vya ardhi na wale wamekaa sehemu hizo kwa miaka nenda miaka rudi wakanyimwa ardhi. Nikisema hivi haimaanishi watu hawatakubaliwa waende kukaa kwa ardhi. La! Tunasema watu waangaliwe vile watakavyo kaa katika ardhi zao. Watu waangaliwe vile wale wamekaa katika ardhi watafaidishwa na hivyo vipande vya ardhi. Tumeona dhuluma zimetendewa watu katika vipande vya ardhi ambavyo vilikuwa vyao. Tukiangalia kama sehemu ya Kaloleni Voi, ni jambo la aibu kuona vile mambo yako. Sheria hii ingekuwa imepitishwa hapo awali watu wa Kaloleni Voi hawangepatwa na dhiki ambayo inawapata hivi sasa. Walitoa ardhi wakiamini wameitoa kwa kiwanda cha Bata kijenge mtambo wa viatu. Baadaye Bata haikujenga lakini ilikuwa imepata stakabadhi za kumiliki ardhi hiyo. Iliamua iuze ardhi hiyo kwa mtu mwingine. Hivi sasa watu wa Kaloleni wanapata shida, na jambo hili linaleta dhiki. Sheria hii ingekuwa imepitishwa tangu hapo awali ingekuwa mambo kama haya yanaepukwa na watu hawangezozana. Hii mizozo ambayo tunaiona hivi sasa ingekuwa haipo. Unakuta ardhi kama za Mwatate na Mwasima Mbuwa, mzungu yuko na ekari 30,000. Wenyeji wamekubali huyu bwana yuko na ekari 30,000. Kwa sababu hii sheria haikuwepo inaonekana waziwazi ametamba akaingia katika ardhi ya wananchi. Akiambiwa ipimwe, inaleta zogo kwa sababu hawataki ipimwe. Ukweli wa mambo ni kuwa kama itabainika waziwazi na Ripoti ya Bunge ambayo imekuja hapa ikasema ardhi hiyo ipimwe kwa sababu imeingia katika ardhi ya wananchi--- Wenyeji wakisema ardhi ipimwe na Kamati ya Bunge imesema ardhi ipimwe, unakuta watu wanazungushana kizungumkuti hawataki ipimwe. Sheria hii ikipitishwa haya malumbano yote yataisha kwa sababu watu watajua haki zao za ardhi ziko wapi. Watu wataweza kuhifadhi ardhi yao na watu wataweza kujua wanalindwa na sheria kuhusu ardhi. Sheria hii ikipitishwa itakuwa rahisi wale watu ambao wako katika sehemu fulani kujua rasilimali yao inaweza kupata malipo ya fidia kiasi fulani. La tusipofanya hivyo, kutakuwa na shida. Mwenzangu amezungumzia misitu. Hii misitu ambayo ni ya wananchi, hivi sasa ilikuwa inatumika kiholela. Lakini sasa ikiwa ardhi hiyo ambayo ni ya wenyeji itarudishwa kwa wenyeji inamaanisha wenyeji watakuwa na mamlaka ya kuweza kusema: “Hii ni misitu yetu. Tutaipangia hivi na vile na tutaweza kuivuna kulingana na msimu huu na faida itakayopatikana itakuwa ni yetu” Hivi sasa unakuta kwa sababu moja au nyingine wananchi ambao wanakaa sehemu hizo na maadamu hawana stakabadhi, ardhi hiyo imekuwa inashughulikiwa na serikali za kaunti. Tukiangalia ule ukora unaoendelea katika serikali za kaunti nyingi si ajabu utakuta wananchi ambao ni wenye kumiliki hiyo ardhi wananyanyaswa na wananyimwa haki zao. Mara nyingi unakuta wajane ambao wamekaa katika ardhi ambao wamepewa vipande hivyo kulingana na sheria za wenyeji, baadaye wanafurukishwa. Hii ndiyo maana sheria hii ya Ardhi za Wenyeji ikipitishwa itakuwa imeokoa wenyeji kwa kiwango kikubwa kuliko vile hali ilivyo hivi sasa. Suala litakuwa: Serikali za kaunti zitakuwa na umuhimu gani kuhusu ardhi hii? Serikali za kaunti zitakuwa hazina mamlaka kwa vyovyote kuhusu ardhi ya wenyeji. Ardhi hii ikishapewa wenywe ni wao waamue kama wanataka kuitenga ama kutoa sehemu fulani ya ardhi hiyo waipatie kwa sababu fulani, labda ni kujenga shule, kiwanda au hospitali. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}