GET /api/v0.1/hansard/entries/625943/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 625943,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/625943/?format=api",
"text_counter": 597,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Hivi ilivyo, wale ambao wanaongoza kaunti wanaweza kuamka asubuhi wakasema: “Hapo tumeamua sehemu hiyo ya ardhi inachukuliwa na inafanyiwa hivi na vile” na wenyewe hawana habari wala fahamu. Hawajaulizwa ama kuombwa. Mara nyingi unakuta sheria hii tukiangalia vipengele kadha wa kadha, na tumevichunguza, moja ya matatizo ya sheria hii nikuhusu dhuluma ambazo zimetendwa hapo awali. Kwa kizungu zinaitwa historical landinjustices. Tunaomba Mswada huu upitishwe na marekebisho, maanake kuna marekebisho ambayo tunahitaji kuyaleta, ili wale watu ambao wamedhulumiwa kwa ardhi zao wapate haki. Ile dhuluma nazungumzia ni dhuluma kama ile imefanyiwa watu wa Taita Taveta; ardhi yao ikachukuliwa ikafanywa mbuga za wanyama, tena wakapokonywa ile sehemu nyingine iliyobaki. Kwa mfano, sehemu kutoka Mackinnon Road hadi Voi chini yote imeenda kwa KWS; mwaka wa 2009 ndio walipatiwa stakabadhi. Waliomba ruhusa kwa nani? Katika sehemu za Kishushe mpaka mto Tsavo, wamekuja wakachukua hiyo ardhi na si yao. Ndio maana tunaomba Mswada huu upitishwe, tukiufanyie marekebisho ili tuhakikishe kwamba ardhi za wenyeji zinalindwa kikamilifu na hazitumiwi kiholela bila mpangilio. Wale ambao wamekuwa huko ndani wapatiwe nafasi yao ya kuishi na kupata stakabadhi za kumiliki sehemu hizo."
}