GET /api/v0.1/hansard/entries/625973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 625973,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/625973/?format=api",
"text_counter": 627,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi nichangie Mswada huu. Ningependa kumshukuru aliyeleta Mswada huu. Watu wanateseka sana kwa sababu ya mambo ya ardhi. Kila ardhi ina mwenyewe lakini hakuna sheria ya kuilinda. Vita vyote vinasababishwa na ardhi na mipaka. Wananchi wanajua mipaka yao lakini kwa sababu ya ukosefu wa sheria ya kulinda ardhi, tuna vita vingi. Nikizungumzia kuhusu Kaunti ya Samburu, tuna “ardhi dhamana” na ni vigumu kujua wanaomiliki ardhi hiyo ilhali watu wanaishi hapo. Vile vile, tuna misitu na wananchi wanaishi hapo kutoka wakati Uhuru ulipopatikana na hawajui wataenda wapi. Hawawezi kulima, kulisha ng’ombe au kujenga kwenye ardhi hiyo dhamana. Naunga mkono sheria hii ili isaidie watu wote wajue kuishi kama wananchi wa Kenya. Sheria hii pia iangalie mipaka ya wananchi. Vita vyote husababishwa na mipaka. Sheria hii pia iangalie wale ambao wanaishi msituni na hawana ardhi. Mara kwa mara, watu hawa wamepewa barua za kuwaambia waondoke kwenye misitu hiyo. Mimi pia nimelelewa kwenye misitu hiyo na wazazi wangu hawana ardhi. Sheria hii iangalie wale watu ambao hawana ardhi ya kuwazika wapendwa wao. Unyakuzi wa ardhi unafanyika kila mahali nchini. Wakati mwingine unasikia ardhi iliyotengewa shule au hospitali imenyakuliwa."
}