GET /api/v0.1/hansard/entries/627075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 627075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/627075/?format=api",
"text_counter": 709,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Vile vile, tukiangalia sehemu za Aldina, Ganahola na sehemu nyingi za eneo Bunge langu, tutapata kwamba kuna matatizo kama hayo. Jambo zuri ambalo ningependa kulisema ni kuyataja yale mambo ambayo ndugu yangu Mhe. Wesley Korir aliyazungumzia jana. Wengi wa mabwenyenye wanahamia kwenye sehemu wanakoishi jamii. Unamwona mtu ako na karatasi ya hati miliki lakini ukimuliza mahali anakuja kumiliki hata hajui. Kwa hivyo, Mswada huu ukipita utapeana haki sawa na utapeana haki za zile jamii ambazo zinaishi katika sehemu zao zisikizwe kwa jambo lolote ambalo litafanyika. Ninasema hivi kwa sababu katika eneo langu la Jomvu na Pwani nzima, shida za ardhi zimekithiri. Ukiangalia kama Aldina, Tume ya Ardhi iliwaita wenyeji. Bw. Swazuri alisema ni lazima yule anayedai ardhi ni yake ajitokeze. Alishindwa mtu yule kujitokeza na mpaka sasa watu wale hawajapata hati miliki za ardhi. Kupitishwa kwa Mswada huu ni muhimu kwao ili wapate hati miliki za ardhi."
}