GET /api/v0.1/hansard/entries/627079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 627079,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/627079/?format=api",
"text_counter": 713,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Mimi pia ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu ni wa maana sana, haswa kwa sehemu yangu ya Trans Nzoia. Tumekuwa na shida kwa sababu ya maskuota katika eneo hili. Vile mwenzangu amesema, tunao watu wanaosema kwamba mzazi wangu alizikwa hapa na hakuna ukweli kwamba hilo shamba linahusu mzazi wake au jamii yake. Kuna watu wengi ambao wanapata taabu katika nchi yetu ya Kenya. Mwenzangu Mhe. Wesley alipoongea jana, alitaja kwamba kuna shida katika Cherangany, eneo la Trans Nzoia. Watu wanakaa mahali ambapo walipelekwa na viongozi waliotaka kupita uchaguzi. Baada ya kupita, wanawaacha hapo wakiwa hawana mahali pa kukaa. Mswada huu utasaidia watu wengi, wakiwemo watu kutoka jamii maskini na wanyonge. Ninakumbuka wakati moja kuna jamii ambazo zilihamishwa kutoka sehemu za Kiboroa kule Trans Nzoia na wengine hawana makao mpaka wakati huu. Tunataka haki itendeke kwa Wakenya wote. Wakiwa na makao yao, hawatabaki kuhangaika na usalama katika nchi yetu ya Kenya utakuwa mzuri. Sisi katika Bunge hili tumekuja hapa kwa ajili ya kuhudumia watu wetu kule nyumbani. Tukishirikiana pamoja na tuupitishe huu Mswada, utatusaidia katika mashinani na hatutatumia watu wetu kwa njia mbaya. Wengine wameongea kuhusu vitambulisho. Lazima uwe na kitambulisho ndiposa upewe hati miliki ya ardhi. Kitambulisho chako kikiwa na dosari huenda ukaambiwa hawajui mahali unatoka. Sasa unaona kwamba lazima hawa watu wawe na vyeti kamili vya mashamba yao au shamba la jamii. Inafaa wakati huu wa kutengeneza Bajeti tuhakikishe kwamba Serikali imepata pesa ndiposa ishughulikie haya mambo ya mashamba ya jamii. Serikali ikitenga pesa fulani za kuhakikisha kwamba inakamilisha shida hizi, itatusaidia sisi kama jamii. Pia, tuna wakimbizi wa ndani ambao walitolewa kutoka kwa mashamba yao. Iwapo huu Mswada utapitishwa, hata wao pia watapata haki zao. Watu wanauliza; iwapo tuko na wakimbizi wa ndani, nani alichukua mashamba yao? Hii ndio sababu tukipitisha Mswada huu, utatupatia nafasi nzuri ya kuhakikisha kwamba kila mtu anapata haki katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hayo machache, asante sana. Ninaunga mkono Mswada huu."
}