GET /api/v0.1/hansard/entries/627717/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 627717,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/627717/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Ningependa kusema ya kwamba Mswada huu umetambua walemavu, akina mama na jamii ya watu wadogo wadogo yaani marginalised community kuwa ni lazima wapate haki sawa sawa. Katika kipengele cha 31 cha Mswada huu, kinasema kuwa kila mmoja ana haki sawa ya kumiliki ardhi katika ardhi za kijamii. Kwa hivyo, Mswada huu unawapatia nguvu wale wakaaji ama wenyeji ambao wako katika ardhi hizo katika maamuzi yoyote yanayotaka kufanyika katika ardhi hizo. Vile vile, tunaona kuwa ikiweza kufanya hivyo, itaweza kutoa nguvu kuwa jambo lolote, hata likiwa ni la kuekeza, watu wenyewe washauriwe halafu kisha baada ya kuweka maamuzi, ndio tuone kwa namna gani mipangilio ile itaweza kufanywa."
}