GET /api/v0.1/hansard/entries/627721/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 627721,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/627721/?format=api",
"text_counter": 269,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Huu Mswada unatupa nguvu kuona kuwa wale mabwenyenye ambao wanakuwa na makaratasi ya kumiliki ardhi na wenyeji wakiwa wanaishi mahali hapo hapo, itaweza kuwapokonya nguvu. Pia, nikiangalia hali hii ya wenyeji, ni lazima wahusishwe. Ni muhimu kwa shauri nikiangalia mradi mkubwa sana wa reli unaofanyika, watu katika sehemu yangu ya Maganda, ambapo inapitia walipewa makaratasi, yaani allotment letters kusubiri hati miliki zao. Unaona mradi ule unafanyika, mtu anapigiwa hesabu za nyumba yake, lakini hapigiwi hesabu ya ardhi. Jambo kama hilo si jambo la sawa sawa. Ni muhimu sana watu watambue wenyeji na wawapatie hati miliki za ardhi ili ziwafanye kuwa na nguvu ya kudai haki yao katika sehemu hiyo. Tukiangalia jambo kama hili, limetuadhiri Pwani nzima. Watu wengi katika jamii zao wanasongezwa kando na wale wawekezaji. Hatimaye, watu kama hao hawapati haki yao."
}