GET /api/v0.1/hansard/entries/629506/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 629506,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/629506/?format=api",
    "text_counter": 284,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Wacha nifuate mwelekeo wako, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Yangu ni kusema kwamba nchi nyingi zimegombana na zimefanya watu wakawa maskini, haswa wakati mafuta ama gesi imepatikana kwa sababu mikataba inawekwa bila Bunge kuhusishwa. Wakati umefika tukubaliane kama Bunge kuwa mikataba yoyote ambayo itawekwa lazima iletwe Bungeni, hasa hii ya mafuta, kabla lolote kufanywa ili tujue ni nini iko ndani yake. Tunaweza kuwa tunajitia kitanzi. Mara nyingi tumejitia kitanzi. Mikataba imewekwa na baadaye ikiletwa hapa Bungeni, tunajikuta tumejifunga. Hatuna la kufanya na hatuwezi kujitoa kwenye mikataba hiyo. Wakati umefika ikiwa tunatunga sheria, tuhakikishe kuwa tumeangalia wale watu wako na hizo rasilmali wasinyanyaswe. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}