GET /api/v0.1/hansard/entries/629566/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 629566,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/629566/?format=api",
    "text_counter": 344,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naomba kupongeza wenzangu kwa vile tumeangalia Mswada huu kikamilifu na kwa undani. Mwisho, tukakubaliana ya kuwa kile kipengele kilikuwa kinatupatia shida, tumekisawasisha na kukubaliana mwelekeo ni upi. Ni muhimu kama Wabunge tukubaliane na tuone kuwa nchi hii na wananchi wanalindwa kulingana na mali ambayo tumejaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa nayo. Mara nyingi, inatumiwa na wageni na wananchi wenyewe hawafaidiki. Ukiangalia nchi nyingi za Kiafriaka hivi sasa, zina shida kwa sababu ya zile sheria ambazo ziko nazo, haswa kuhusu rasilmali zao. Mara nyingi, wanashikwa mateka na watu ambao wamekuja nchi zao kutafuta mali hiyo. Nashukuru kuwa kama Wabunge, tumewajibika ya kutosha kuhakikisha kuwa tunaweka sheria kabambe za kuangalia kuwa rasilmali za nchi zinalindwa na kuwa wakenya watafaidika kutokana na rasilmali ambazo Mwenyezi Mungu ametujalia. Naomba wakati ufike wa kutekeleza sheria hizi pia ili mikataba itakayowekwa ifuwatiliwe kwa uangalifu. Lazima tuangalie vile sheria zitawekwa ili mikataba isije ikageuka sheria na ikawa sasa ndiyo inatawala kuliko sheria zile tumeweka. Nchi nyingi zimeingia kwenye shida na ningeomba nchi yetu iepuke shida hizo. Tunapitisha sheria hii wakati huu ambao tunaona yale ambao yamepata wenzetu. Kwa hayo mengi, naomba niunge mkono na nipongeze wenzagu."
}