GET /api/v0.1/hansard/entries/630325/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 630325,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/630325/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Asante, Bwana Spika kwa nafasi hii ya kuzungumzia Mswada huu. Ninauunga mkono. Ninaomba upitishwe kwa sababu tumekuwa tukipata shida sana tangu enzi za Uhuru hadi sasa hapa nchini, hususan sehemu nyingi za Mkoa wa Pwani. Uenezaji wa umeme umekuwa ukifuata sanasana barabara za lami. Watu ambao wanaishi karibu na hapo ndio wamekuwa wakipata sitima. Wananchi wengine wamekuwa wakiachwa kwa giza kwa siku nyingi licha ya kuwa na huo mpango wa kuleta stima katika sehemu ambazo ziko ndanindani na ni za mashambani. Bado kuna watu wengi ambao wako nyuma kiuchumi kwa sababu hakuna stima ya kutosha. Pia, inaonekana kama sehemu nyingine zinabaguliwa kwa sababu ya kutopata stima. Mpaka sasa, licha ya kuwa tumesikia Serikali ya Jubilee ikihimiza kuwa shule zipate stima, bado kuna shule nyingi ambazo hazijapata stima. Hata kama kuna wafadhili ama walimu ambao wanataka kuendeleza masomo, hususan ya tarakilishi kuendelesha watoto au kutumia video au runinga kuwaelimisha watoto, haiwezekani. Kwa hivyo, unapata watoto wengi ambao wamesoma sehemu za mashambani, kama huko kwetu Kwale, wameshindwa kupata masomo ya hali ya juu. Hii ndio maana unaona mara kwa mara katika masuala ya matokeo ya mitihani ya shule za upili au za msingi, huwa si mazuri sana kwa sababu ni kama wametengwa wao pekee na hawako pamoja na wenzao. Pia, biashara zimeathirika sana kwa sababu ya kukosekana kwa umeme. Vijana wetu pia wameachwa kando. Lakini ninaona sheria hii itajaribu kurekebisha mambo haya ili nchi nzima iendelee. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu."
}