GET /api/v0.1/hansard/entries/630354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 630354,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/630354/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Jambo ambalo tunahitaji kulizingatia ni kwamba ni lazima kuwe na mwelekeo wa kupunguza umaskini katika nchi yetu. Naamini kwamba umeme utakapokuwepo, viwanda vingi ambavyo vinatumia umeme vitalipa pesa kidogo ili bidhaa kutoka kwa viwanda hivyo ziweze kuuzwa kwa bei nafuu na wananchi wapate huduma ambazo zitawasaidia kujitoa kutoka kwa umaskini. Bidhaa nyingi hivi sasa zimekuwa na bei ya juu kwa sababu zinatumia umeme ambao ni wa bei ya juu sana. Hayo ndiyo matarajio makubwa ambayo tunahitaji kuwa nayo tunapolizingatia suala hili."
}