GET /api/v0.1/hansard/entries/631257/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 631257,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/631257/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Nataka kutoa maoni yangu kuhusu dua la pili kutoka Kaunti ya Laikipia kuhusu elimu ya chekechea. Ni jambo la kusitikisha kwamba kuna mtafaruku sana kuhusu elimu hii. Hii ndio inawapa watoto wetu kama ilivyofanya kwetu msingi ambao unatuongoza maishani. Kaunti zingine zimetoa tangazo kwenye magazeti kwamba watu waombe hizi kazi. Ni lazima tutatue mtafaruku huu kwa haraka ili watoto hawa wapate masomo. Jambo la pili ni lazima kamati ya Seneti inayoshughulikia masuala ya elimu izingatie madarasa watoto hawa wanasomea. Ukizuru shule nyingi utaona darasa mbovu ndilo watoto hawa husomea. Madarasa mengi huwa ni ya matope. Hawana vyoo bora na hupatwa na magonjwa ya kila aina. Kila asubuhi, watoto hawa hulia kwa sababu hawataki kwenda shuleni. Hakuna jambo linalowavutia kwa shule. Elimu hii ni muhimu sana. Ni lazima tuhakikishe kuwa madarasa yao ni ya hadhi ya juu na ya kuwavutia watoto wetu. Mwisho, natumai kwamba Mswada wa Elimu ambao uko mbele ya Bunge la Kitaifa utaletwa hapa ili tuujadili na kuupitisha ili tutapate suluhisho ya mambo haya."
}