GET /api/v0.1/hansard/entries/632233/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 632233,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/632233/?format=api",
    "text_counter": 256,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Shakila Mohamed",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Mswada huu muhimu kuhusu swala la ardhi. Swala la ardhi ni nyeti sana. Ningetaka nichukue nafasi hii kuipongeza Kamati ya Ardhi kwa kazi nzuri waliyoifanya kuleta Mswada huu kuona kwamba tutasonga mbele kutokana na mashaka ya ardhi tuliyo nayo. Ardhi ni swala nyeti sana na lina changamoto nyingi sana. Hivi sasa, kuna sehemu nyingi hususan upande wa Pwani ambako kumekumbwa na dhuluma nyingi sana za mashamba ambazo tunaamini huu Mswada ndio utaleta suluhisho kwa shida kama hizo. Kuna umuhimu Mswada huu, uangaliwe kwa makini na upigwe msasa zile sehemu ambazo zinafaa ili ukiwa utatekelezwa kwa wananchi, basi uwe ni Mswada unaoweza kunufaisha Mkenya popote pale alipo na sio Mkenya kutoka sehemu fulani awe atazidi kuumia. Madhumuni na malengo ya Mswada huu ni kumaliza zile shida ambazo zimetukabili katika mambo ya ardhi, hasa zile sehemu ambazo kufikia sasa kuanzia tupate Uhuru nchini Kenya, bado zinakumbwa na changamoto. Mswada huu uko hapa kulingana na Katiba yetu ambayo tuliipigia kura tukitarajia kwamba Mswada huu ndio kitu ambacho kitakuja kutumalizia shida zetu za ardhi. Kifungu 44(15) kinataka kuondoa mamlaka ya Tume ya Kitaifa ya Maswala ya Ardhi (NLC), ambayo imetengenezwa na Katiba na imepewa uwezo kuangalia tuhuma za mashamba ambazo zinaendelea katika nchi hii. Tunasikitika ikiwa NLC itapokonywa uwezo na nguvu ya kutekeleza majukumu yake kulingana na katiba. Basi bila shaka, kama nchi tutakuwa tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele--- Hatutaki tena kujikuta tuko nyuma kutokana na ile shida ambayo ilikuwa inatukabili. Wananchi wako kwenye ardhi zao wakijua huku ni kwao. Wengine huku juu wameshikilia vyeti vya mashamba wakisema kwamba hizo ardhi ni zao. Tunataka vile wananchi walivyotoa mapendekezo yao kwamba kuwe na NLC, iwe itaangalia shida kama hizo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}