GET /api/v0.1/hansard/entries/632234/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 632234,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/632234/?format=api",
"text_counter": 257,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Shakila Mohamed",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Mapendekezo ya wananchi ni kwamba ugawaji wa ardhi utoke mashinani kwenda juu na si kutoka juu kwenda chini kama ilivyokuwa zamani. Vile Mswada huu unavyoelekea, unaturegesha nyuma kule tulipotoka. Mswada huu unataka kupokonya nguvu NLC na kuzipatia kwa Wizara ya Ardhi ambayo ilikuwa na majukumu haya na dhambi nyingi zilitokea kulingana na haya majukumu ambayo walikuwa nayo wakati huo. Hatutaki tena kuona zile dhambi zikiendelea. Tunataka kuumaliza ule msururu wa dhambi. Tunataka kuona kila mmoja amepata haki yake ya kikatiba na kila mmoja amepata usawa kama wengine. Hatutaki kuona dhuluma wala mambo ya misururu ya kunyanyasana ikiendelea kwa upande wa ardhi. Tunataka kuona maendeleo. Tunasikitika kuwa Serikali tulionayo inataka kuturudisha nyuma kwa kupitisha Mswada ambao unapokonya NLC mamlaka ambayo imepewa na Katiba kupitia kwa kura za wananchi na kuregesha haya mamlaka kwa Wizara ya Ardhi ambayo ilisababisha dhambi na shida ambazo zinatukabidhi kama wananchi wa Kenya. Kwa hivyo, tunataka huu Mswada, kabla haujapitishwa, upigiwe msasa na uwe ni Mswada ambao utaweza kuwahudumia Wakenya wote. Unafaa kupeana muongozo na mwelekeo kwa kila Mkenya bali si kwa baadhi ya Wakenya."
}