GET /api/v0.1/hansard/entries/632246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 632246,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/632246/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii nikiwa mmoja wa wanakamati wa Kamati ya Ardhi, kuzungumza kuhusu Mswada huu wa swala nzima la ardhi ambalo limeletwa hapa Bungeni. Ningependa kuipongeza Kamati kwa juhudi zake na yale ambayo wameweza kufanya mpaka kufikisha huu Mswada hapa. Utakubaliana nami ya kwamba swala la ardhi nchini ni nyeti na halihitaji kujadiliwa kiufupi ama kwa namna isio sawa. Hivi sasa Wakenya wengi wana hamu kubwa kujua swala hili limekuwa na mwelekeo upi katika nchi yetu ya Kenya. Tukiangazia pakubwa, Wakenya walipigia Katiba kura na wakaweka Tume ya Ardhi ili kutatua na kusawazisha swala la ardhi. Swala hili limeonekana kuwa ligumu na nyeti kwa siku nyingi sana kuanzia nchi hii ilipopata Uhuru. Haitakuwa sawa kwa Bunge kujadili mambo haya ambayo yana undani sana kwa namna ambao si sawa. Kwa kweli, Mswada huu umechanganya mambo mengi sana haswa yale ya dhuluma za kihistoria. Wengi walipatwa na maovu haya na dhuluma hizi za kuhusiana na mswala ya ardhi. Vile vile, Mswada huu umechanganya mwongozo ambao utapatikana kuhusu hili swala na majukumu ya Wizara na tume. Kwa kweli, ningependelea pakubwa swala nzima hili, kuanzia maovu ambayo yalifanyika kuhusu ardhi hapa nchini, liangaliwe. Hili ni swala ambalo in gumu sana na hivi sasa lina utata mkubwa. Wakenya wengi katika kila pembe ya nchi hii, haswa wa Pwani, wamedhulumika pakubwa na swala hili. Matatizo mengi ambayo tunayaona kuhusiana na ghasia na mengineo ni kutokona na tatizo la ardhi. Watu wengi wamedhulumiwa na hawajapata haki zao kuhusiana na maswala ya ardhi. Walipokonywa ardhi na mababe kwa sababu ya uzoevu ama hali ya kiuchumi. Utapata mtu ana ardhi yake lakini kwa sababu hana uwezo wa kufuatilia stakabathi, mwenye uwezo anapata hizo stakabathi. Ningependelea pakubwa kama swala hili la watu walio dhulumiwa katika mswala ya ardhi litajadiliwa. Lisichanganywe na mswala mengine. Hivi sasa, watu wengi wamepatwa na janga hili na tukiangalia dhuluma ambazo zimefanyika, haswa nikizungumzia Pwani, ni asilimia themanini. Tutawezaje kujadili swala hili pamoja na mswala mengineo katika mwongozo mzima wa ardhi? Sioni sababu ya sisi kupitisha Mswada huu wakati kuna mengi yamechanganywa. Hivi sasa, Wakenya walikuwa na imani kubwa sana na Tume la Ardhi kutatua swala hili. Inaonekana kama tume hii inapokonywa mamlaka yake na kupelekwa kwa Wizara, kinyume na mapendekezo ya Wakenya. Mara kwa mara nikiwa katika Kamati ya Ardhi, kuna malalamiko kutoka kwa tume hii. Wanakuja kwa Kamati na kulalamika kuwa hawapewi uhuru wa kufanya kazi yao na Wizara. Pia, wanalalamika kuwa kuna baadhi ya stakabadhi ambazo wanahitaji ili kutatua matatizo haya ya ardhi kupitia kwa Wizara ambazo wananyimwa. Pia, kuna maelezo ambayo yatawasaidia kuendesha kazi zao. Katita hali hii, inaonekana wazi kwamba swala nzima la ardhi, Wakenya walipendekeza lielekee mwelekeo huu, lakini Serikali, Wizara na Tume ya Ardhi hawajakuwa na mwongozo kikamilifu kumsaidia Mkenya wa kawaida. Nimelishuhudia tatizo hili mara nyingi baina ya Wizara na Tume la Ardhi. Ni vipi Mmkenya wa kawaida atasaidika na ilhali kule kuna matatizo? Mwongozo ambao tuko nao hapa Bungeni kuhusiana na swala la ardhi, ningeomba Wabunge wenzangu wahakikishe kwamba tumelijadili inavyotakikana, tulishambue kila jambo na kuliweka mahali pake. Hofu yangu ni kwamba Mswada umechanganya mambo mengi. Katika Bunge hili, kile ambacho nimeona ni kwamba ni Waheshimiwa wachache ambao hupitia Mswada kama huu ili kujua umesema nini au una mwongozo gani. Lakini kama Mwanakamati wa Kamati ya Ardhi, Mswada huu una matatizo mengi. Wakenya wana imani kubwa kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}