GET /api/v0.1/hansard/entries/633070/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 633070,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/633070/?format=api",
    "text_counter": 508,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Natumaini muda wangu unaangaliwa usije ukaisha kwa sababu ya shughuli za kuangalia nani amezungumza na nani hajazungumza. Kisiwa cha Migingo ni sehemu ya Kenya. Mimi ni Mkenya na nawakilisha sehemu ya Wundanyi ya Taita Taveta ambayo ni sehemu ya Kenya. Sehemu yoyote ya Kenya ikiguswa na mtu yeyote, nina haki ya kuzungumza kuhusu jambo hilo na kutoa mchango wangu. La pili, tumesikia na tumeelezwa kuwa mara nyingi Hoja zimeletwa hapa Bungeni kuhusu Kisiwa cha Migingo lakini hakuna lolote linalofanywa. Watu wanaumia, wanauawa, wananyang’anywa mali yao na Serikali yetu inaangalia. Kulingana na maoni ambayo yametolewa hapa leo, tumeelezwa kuwa kulikuwa na tume ambayo ilienda Uganda, ikajadiliana na Serikali ya Uganda na wakakubaliana kuwa masoroveya wapime, waangalie, wafuate utaratibu na wajue hii sehemu ya Migingo iko sehemu gani. Walikubaliana baadaye kuwa Migingo iko upande wa Kenya. Serikali ya Uganda ikakataa kuweka sahihi makubaliano hayo. Baadaye, Serikali ya Kenya ikaanza kuongeza biashara na wao. Ni kwa nini tunabembeleza Uganda? Ni nini wanachotupatia ambacho kinatufanya tubembeleze Serikali ya Uganda? Hata wakati wa hayati Rais Amin, mnakumbuka vitisho alivyotupatia lakini Serikali ya Kenya ilitoa ukali ikaiambia kuwa “hebu jaribu na tutaona ni nini kitafanyika”. Walipojaribu kuvamia Tanzania, Mhe. Mwalimu Kabarage Nyerere alitoa jeshi lake likaenda likakomesha Uganda. Sisi watu wa Kenya tunaendelea kulalia masikio. Hata hivi tulivyo, si Migingo peke yake. Hata Somalia imeanza kusema ufuo wa bahari upande wa Lamu kuenda ndani mpaka kilomita 200 ni sehemu yake. Kenya bado inatapatapa. Hatujui kama kesho sehemu ya Tanga, upande wa chini wa Mombasa, itapeanwa nchi nyingine. Wakati umefika wa Serikali ya Kenya kuamka na kusema waziwazi kuwa hatutavumilia watu wetu waendelee kuteswa, kunyanyaswa na kudhulumiwa katika Kenya. Tukiwa na shida kama hizo, na Majeshi yanatakiwa yalinde mipaka yetu, tunashangaa ni kwa nini tusishugulikie mambo kama hayo ya mipaka badala ya kutuma magari na Wanajeshi kwa uchaguzi mdogo wa Malindi. Hata haya hatuna. Tuko tayari kuzozana sisi wenyewe na kunyang’anya magavana wetu silaha zao ambazo wanazitumia kwa ulinzi wao. Ndio maana tunasema haki ifanyike. Tufanyie watu wa Migingo haki na watu wetu hapa nchini tuwafanyie haki. Mambo kama haya tunayaona The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}