GET /api/v0.1/hansard/entries/633129/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 633129,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/633129/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wangari",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13123,
        "legal_name": "Martha Wangari",
        "slug": "martha-wangari"
    },
    "content": "Nakushukuru, Bw. Spika. Nachukua nafasi hii kumkaribisha Sen. Aaaron Cheruiyot katika Seneti hii. Nderemo na vifijo katika Seneti hii ni dhihirisho tosha kuwa Sen. Cheruiyot ni mashuhuri sana katika Kaunti ya Kericho. Hatuna shaka kuwa atawaakilsha vilivyo wananchi wa hiyo kaunti na Kenya kwa jumla. Ningetaka kumpongeza aliyekuwa Seneta wa Kericho na sasa ni Waziri wa Kawi kwa kazi yake nzuri. Hatuna budi kuwa atafanya kazi nzuri katika Wizara ya Kawi. Ningetaka kumkaribisha Sen. Cheruiyot kwa kikundi cha “Vijana wa Bunge”. Sisi ni Wabunge chipukizi kutoka Seneti na Bunge la Kitaifa ambao umri wetu ni kati ya miaka 18 na 35. Kikundi hiki kina waheshimiwa Wabunge 47. Sasa tumefika 48. Ninakukaribisha kwa moyo mkunjufu katika kikundi hiki ambacho huongozwa na Mwenyekiti wa TNA, Mhe. Sakaja. Sisi katika kikundi hiki hatuna mipaka kati ya Bunge zetu mbili. Ningetaka kuwashukuru watu wa Kericho kwa kufanya uchanguzi wa haki na amani. Hatukushuhudia vituko au vita kama mahali kwingine. Hatukuwaona wanawake walio vuliwa nguo kama ilivyofanyika kule Malindi. Hawa ni watu wa heshima. Ningetaka kuwahimiza waendelea na moyo huo ili tujenge nchi yetu."
}