GET /api/v0.1/hansard/entries/634118/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 634118,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/634118/?format=api",
"text_counter": 199,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Kwa kweli kumekuwa na tatizo kubwa katika suala la umeme katika nchi yetu. Tunajua vizuri kwamba kampuni ya Kenya Power and Lighting Company ndiyo iliyokuwa ikishughulika sana na suala hili na wao ndio washikadao katika suala la kusambaza umeme katika nchi yetu ya Kenya. Wachache ndio walikuwa wakipata huduma hii na wengi hawakuwa wakiipata. Kumekuwa na matatizo makubwa sana kwa sababu ukilinganisha na matumizi, utaona kwamba malipo ya huduma hiyo yako juu. Kutokana na hali hii, kumekuwa na utata mkubwa lakini nimeshukuru pakubwa kwamba jambo hili limeweza kusambazwa kwa njia nyingine kiasi kwamba kumekuwa na mashirika mengine ambayo yanasambaza umeme."
}