GET /api/v0.1/hansard/entries/634123/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 634123,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/634123/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ni lazima Serikali pia iwajibike pakubwa kuhakikisha kwamba wananchi wamelindwa. Utapata mashirika mengi ya umeme yanapata hasara fulani ama kunatokezea mambo ambayo yanaleta kutokua na mwelekeo katika suala hili. Ningependa Serikali iwe na tahadhari kubwa kwa sababu kuna malalamishi mengi juu ya suala hili kutoka kwa wananchi. Mara nyingi wananchi hulalamika kuhusu huduma duni wanazopata kutoka mashirika kama haya. Wakati mashirika kama hayo yanapokwenda kwenye sehemu kama hizo, kuna mambo fulani ambayo wananchi wanatarajia yazingatiwe pakubwa, haswa masuala ya ajira. Watu kutoka sehemu nyingine hupelekwa kufanya kazi katika sehemu hizo lakini wenyeji ndio wanaostahili kupewa kipaumbele kwenye masuala ya ajira. Vilevile, kuna masuala mengine. Wakati huduma hiyo inapofika katika eneo hilo, wenyeji wanastahili kuzingatiwa zaidi kuliko wageni."
}