GET /api/v0.1/hansard/entries/635302/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 635302,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/635302/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Hassan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 431,
        "legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
        "slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
    },
    "content": "Nidhamu, Bw. Spika wa Muda. Nimekuwa nikimsikiliza Seneta wa Lamu ambaye ametoa shutuma katika maongezi yake. Hili ni Jumba la itifaki na lazima uwe na ithibati kwa kila jambo unalosema. Amesema kwamba Gavana wa Lamu alichochea maskwota na kuwaambia wafanye vitu fulani. Ni shutuma kubwa kusema kuwa Gavana anaporomosha maendeleo. Sisi hapa, katika Sheria zetu za Seneti, tunasema kuwa huwezi ukataja mtu kwa namna mbaya bila ya kutoa ushahidi ua kuthibitisha kile unachosema. Kwa hivyo, ningependa ndugu yangu ambaye ni mzee wetu na sote wapwani tunamheshimu, akithibitishe shutuma hizo ama aziondolee mbali. Nimefundishwa Kiswahili na Kiongozi wetu, Sen. Wetangula."
}