GET /api/v0.1/hansard/entries/635329/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 635329,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/635329/?format=api",
"text_counter": 324,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika, ninashukuru sana kwa nafasi hii niweze kuunga mkono majina ya waheshimiwa waliopendekezwa kuhudumu katika Kamati hii ya maana sana. Ninamshukuru sana Mheshimiwa (Dr.) Khalwale kwa kazi tangulizi aliyofanya wakati alikuwa Mwenyekiti. Alifanya kazi yake bila uoga wala shauku. Alitumikia taifa na kuleta Miswada hapa Bungeni kuangalia kwamba mali ya umma inatumika vizuri. Sote tunaamini kwamba uzembe na kuharibu mambo katika taifa letu umeenea katika sekta zote. Wakati Rais Uhuru Kenyatta alipozuru nchi ya Uyahudi, alisimama na kuongea na Wakenya huko. Badala ya kuwapa salamu na kuwaeleza jinsi Wakenya tunavyoishi--- hakuweza kupata matamshi hayo. Hayo maneno hakuyapata katika fikira zake. Alienda moja kwa moja na kusema kwamba taifa letu ni kama limebarikiwa kwa baraka za jinsi ya kuiba. Bw. Spika wa Muda, wanaoharibu na kuiba sio wageni kutoka nje. Ni watoto wetu wanaosomeshwa na mali ya umma, wazazi wao ni mali ya umma, wanawasomesha lakini mwisho inakuwa ni patashika. Kwa hivyo, ni matumaini yangu kama kiranja wa bunge ambaye nimesimama hapa, na niliweza kuchangia kuleta majina ya watu watakahudumu katika kamati hii, kwamba watakaokuja watafuata nyayo za Sen. (Dr.) Khalwale kwa sababu sisi hapa tunaweza kupiga kura moja kwamba kuna waliojaribu kumhonga Sen. (Dr.) Khalwale asiweze kuwakashifu lakini alikataa na huo ushaidi upo. Kwa hivyo, wanaoingia sasa waangalie, watunze na wafanye kazi ya wananchi. Bw. Spika wa Muda, kazi na hesabu ya kaunti, ni ya kaunti ya kila mtu hapa. Jambo la kushangaza ni kwamba, nimetembea katika sehemu mbalimbali ya taifa letu na nilianzia kwangu Machakos na nilifikiria gavana wangu ndiye tu akifanya mradi hata kama ni nusu au robo, anabandika kibao na picha yake hapo. Katika hesabu ya pesa za umma zilizotolewa kuenda katika kaunti, hakuna maksio ya kwamba gavana aweke kibao. Magavana wamekosa heshima kwa sababu wantatumia pesa wanazopewa kutumia kwa wananchi kutengeneza vibao kwa zaidi ya Ksh200,000. Hiyo pesa inatumika kufanya siasa zao pia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}