GET /api/v0.1/hansard/entries/635331/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 635331,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/635331/?format=api",
"text_counter": 326,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, tufikirie hapa. Kama hayati Mzee Jomo Kenyatta angelikuwa anaweka vibao katika miradi iliyofanywa na serikali yake, halafu aingie Moi miaka 24, halafu Kibaki miaka 10, na hatimaye Uhuru miaka mingine 10, kweli tutakuwa na nafasi hata ya kujenga choo katika taifa letu? Nchi nzima itakuwa ni vibao tupu vya kutangaza watu ambao hata mbele ya macho ya Wakenya hawana heshima ata kidogo. Kwa hivyo, ni matumaini na mategemeo yangu kwamba kamati inayokuja, mwenyekiti na naibu wake na wale washiriki wote wawaite hao magavana na kuwauliza pesa waliotumia kutengeneza vibao, waliuza shamba gani au walilipwa mishahara gani au nani aliwapa hizo pesa, kama ni ya ukoo yao au jamii yao? Wanafaa waambiwe waende wang’oe na walazimishwe warudishe hizo pesa walizotumia kutangaza majina yao katika taifa letu kwa sababu hii ni mali ya umma na haifai kutumiwa vibaya. Bw. Spika wa Muda, nikimalizia, nataka kuunga mkono Sen. (Dr.) Khalwale kuhusu maneno aliyosema ya vyama kwamba kamati hii isiingiliwe na vyama na isigawanyike kwa misingi ya milengo ya kisiasa. Kuna watu wanajihisi kwamba wako upande wa Serikali na wengine wako katika upinzani. Bado ni vuta nikuvute katika mazungumzo yetu na majadiliano yetu lakini la muhimu ni kwamba, tunapovutana, ni mwananchi anayeumia. Tunataka usawa ufanyike ili kamati hii itumikie wananchi ili waweze kupata haki yao. Tuliweza kuvurugana upande ule na huu kwa majina, wengine wakahamia huko na wakapata viti huko lakini tunasema sisi sote ni watoto wa mtu mmoja, nchi moja na akili yetu na mategemeo yetu ni kitu kimoja. Naunga mkono."
}