GET /api/v0.1/hansard/entries/635534/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 635534,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/635534/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. William Baraka Mtengo",
"speaker_title": "The Member for Malindi",
"speaker": {
"id": 13164,
"legal_name": "Willy Mtengo",
"slug": "willy-mtengo"
},
"content": "Mhe. Spika, vile vile, ningetaka kushukuru watu wa Malindi, haswa, kwa kunipigia kura kwa wingi: kura za hiari; sio kura za kununua; sio kura za vitisho; sio kura za kutuletea magari ya jeshi wala kutupigia kifua. Nawashukuru wote kwa sababu walijitokeza kwa wingi na wakanipigia kura kwa hiari yao. Kutoka chini ya moyo wangu, nataka niwakongole watu wa Malindi. Vile vile, nataka nimshukuru kinara wa chama chetu, Mhe (Eng.) Raila Odinga kwa mchango wake ndani ya kampeini yangu. Alijitolea kimasomaso. Ningetaka kumshukuru Mhe. Kalonzo Musyoka, Kinara-mwenza ndani ya mlengo wetu wa CORD. Singetaka kumsahau Mhe. Wetangula ambaye alichangia pakubwa, haswa kwa muda wake katika kampeini yetu ambayo ilitupa ushindi mkubwa. Nawaheshimu kwa namna ya kipekee vijana ngangari; vijana wachapakazi na vijana watanashati wa kutoka Pwani wakiongozwa na Mhe. Amason Jefwa Kingi ambaye ni Gavana wetu wa Kaunti ya Kilifi, Mhe. Hassan Ali Joho, Gavana wa Kaunti ya Mombasa, akina mama Aisha Jumwa Karisa, Mishi Mboko na Waheshimiwa wengi ambao nitawataja kwa haraka haraka. Mhe. (Eng.) John Mruttu, Gavana wa Taita Taveta, Mhe. Stewart Madzayo, Seneta wetu wa Kaunti ya Kilifi, Mhe. Rashid Bedzimba, Mhe. Abdullswamad Sheriff Nassir, Mhe. Bady Twalib, Mhe. Omar Mwinyi, Mhe. Kamoti Mwamkale, Mhe. Mwanyoha, Mhe. Zuleikha na bila kumsahau Mhe. Ababu Namwamba, Katibu Mkuu wa chama chetu. Namshukuru Mhe. Sumra kwa muda alioutumia ndani ya eneo langu la Malindi."
}