GET /api/v0.1/hansard/entries/635539/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 635539,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/635539/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Willam Baraka Mtengo",
"speaker_title": "The Member for Malindi",
"speaker": {
"id": 13164,
"legal_name": "Willy Mtengo",
"slug": "willy-mtengo"
},
"content": "Nawahakikishia watu wa Malindi kwamba nitakufa nao kuhakikisha tumeleta maendeleo Malindi ili watoto wa Malindi wasome, wakulima wa Malindi wafanye kilimo chao wanavyotaka, wavuvi wavue samaki watakavyo, akina mama wetu waende kwenye hospitali na zahanati zetu na kupata huduma muafaka, usalama udumike, barabara zijengwe na maendeleo yakithiri. Hayo ndiyo yaliyonileta ndani ya Bunge hili. Mhe. Spika, nasema kuwa sheria zilizoundwa ama zinazoundwa ndani ya Bunge hili la Kitaifa ni sharti zifuatiliwe. Tuliona vitimbi wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi. Mambo hatujawahi kuyaona. Tuliona vitisho, kupigiwa kifua na pesa nyingi, lakini tulichukua msimamo na tukasimama. Nawaambia Wakenya enzi za kuona vitimbi zimepitwa na wakati. Ni sharti tusimame kidete na Kenya yetu iende mbele. Ningetaka kuwaasia viongozi walioshika nyanja hizi katika sekta ya usalama na sekta ya ulinzi wahakikishe kwamba usalama umedumishwa na mwananchi wa Kenya aende kupiga kura kwa uhuru wake katika uchaguzi mkuu ujao. Labda, ningepata kura nyingi zaidi ya hizi isipokuwa ni kwa sababu watu wetu walitishika. Tuliona vifaru vya jeshi vimewekwa nje ya vituo vya kupiga kura. Tuliona askari wengi ambao hatujawahi kuwaona katika sehemu zetu na mambo ya kututisha. Kwa ruhusa yako, ningeomba Waziri anayehusika na mambo haya ayachunguze; yasiwachwe wazi wazi. Tunataka Bunge hili lipate ripoti kamili. Hakuna shida ya usalama Malindi wala tatizo la usalama."
}