GET /api/v0.1/hansard/entries/635543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 635543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/635543/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Willam Baraka Mtengo",
    "speaker_title": "The Member for Malindi",
    "speaker": {
        "id": 13164,
        "legal_name": "Willy Mtengo",
        "slug": "willy-mtengo"
    },
    "content": " Mhe. Spika, singetaka mji wetu wa Malindi ambao ni uchumi wetu, uchumi unaotegemea utalii, uharibiwe sifa. Sasa, ukichukua askari na kuwaweka ndani ya mji wa utalii, si ni kuwatisha? Ujumbe ambao tunatuma upande ule mwingine ni ujumbe wa kutatanisha. Haya ni maswali ambayo ningependelea na kuomba tupate majibu ndani ya Sakafu hii ya Bunge, kama Mbunge wa eneo Malindi. Wale watu walikuja kwa minajili gani? Vifaru vya jeshi siku ya kura tena kando ya vituo vya kupiga kura vililetwa kwa minajili gani? Baada ya vituo kufunga, askari wote walitoroka. Vifaru vingi viliondoka na vichache vikabaki kwa vituo vya kupiga kura. Miongoni mwa watu wangu ambao walinichagua kwa kura nyingi, bado tunapata ripoti kuwa wameshikwa. Wanashikiwa nini? Tunataka tujue. Hata kwa ule upande mwingine, tunajua watu wengi walishikwa na fedha nyingi nje ya vituo vya kupiga kura siku ya kupiga kura. Ambia Wakenya fedha zile ulikuwa unafanya nazo nini ukishikwa nje ya vituo vya kupiga kura siku ya kupiga kura. Ulikuwa unafanya nazo nini kule? Wameachiliwa na wengine waliachiliwa muda mchache baada ya kushikwa. Tunataka majibu. Watu wetu wanataka majibu wakiwa kule mashinani. Nashukuru Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kazi waliyofanya. Sisi si malaika. Tungetarajia hali bora zaidi. Kwa muda ule na yaliyojiri, tunataka tuwashukuru na tuwakongole kwa kazi waliyofanya. Nina imani kwamba watafanya uchaguzi unaokuja vyema wakiboresha huduma zao lakini wana mambo machache ya kurekebisha. Kwa kiwango kikubwa, nawashukuru kwa sababu uchaguzi ule ulikuwa mwema. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}