GET /api/v0.1/hansard/entries/638092/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 638092,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/638092/?format=api",
"text_counter": 589,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nawashukuru Wabunge wote ambao wamechangia Hoja hii na hata ile ari ambayo imekuwepo ya kuweza kuchangia zaidi. Hususan, ningelipenda kuwatambua Architect Kiaraho, Mhe. Abdulswamad na Wabunge wengi ambao wangelipenda kuchangia Hoja hii. Sasa hivi, tumetoka kuzindua kitabu kuhusu mambo ya vijana kutokuwa na ajira. Nimeweza kuandika sura nzima hapa katika hicho kitabu kuhusu vile walemavu wanakosa nafasi za ajira. Jambo hili linatokana na kwamba watu hawana nafasi ya kuingia katika majumba. Hawawezi kupanda maghorofa na hata magari. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuhakikisha kwamba watu wetu wenye ulemavu wanaweza kuridhia katika nafasi zilizoko za umma. Vile ambavyo tunaunda nyumba zetu, tunafaa kuzingatia kwamba leo hii unaweza kuwa mzima wa afya, lakini kesho mambo yanaweza kubadilika. Kwa hivyo, tukiyajenga majumba yetu, tusiwazingatie tu wale walio wazima wa afya bali pia walemavu. Pili, ikiwa tunaweza kutumia asilimia kumi na tano ya Wakenya wenzetu kuchangia mipango ya maendeleo, imaanisha kwamba tutainua hali ya uchumi wetu, tutaendelea kuondoa umaskini na uchochole ili walemavu wajitegemee na wajihisi wenye hadhi. Tunaweza kutunga sheria nyingi katika Bunge hili lakini la muhimu ni kuhakikisha mambo haya yanatekelezwa. Natoa mwito ya kwamba, tuhakikishe kwamba tunafuatilia na tunaweza kukadiria hizo pesa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}