GET /api/v0.1/hansard/entries/638093/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 638093,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/638093/?format=api",
    "text_counter": 590,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Tayari tumekuwa na kikao na Kamati ya Uwiano wa Kitaifa na Usawa wa Nafasi ambayo inaongozwa na Mhe. Johnston Sakaja. Pia, tumeweza kukutana na Kamati ambayo inaongozwa na Katibu wa Wizara ya Miundo Msingi ili waweze kutathmini ni changamoto zipi zipo katika sheria na ni zipi zipo katika utekelezaji ndiposa tuwe na suluhu ya kudumu. Msada huu unatoa mapendekezo mawili. Kwanza, ni kuwa ile Taasisi ya Kitaifa ya Ujenzi ihakikishe kwamba majumba ya umma yote ambayo yataundwa katika, katika ule uchoraji, yazingatie maswala ya watu wenye ulemavu. Pili, ni kutoa ratiba ambayo iko na wakati mwafaka wa kuhakikisha kwamba mambo haya, hatutayazungumzia tu, bali yanaweza kutekelezwa. Ningependa kusema ahsante sana kwa Bunge hili. Ni muhimu kuwa na uwakilishaji wa watu wenye ulemavu katika Bunge hili. Tukija hapa, kuna wale ambao wametufanya tukateuliwa katika viti hivi vya Bunge na tutaendelea kuwatetea kwa sababu sisi ni kama wao. Tungependa kuona hali yao ya maisha imeinuka ili waonekane kwamba hata wao kweli wanafaa katika nchi hii ya Kenya. Nashukuru na ninapongeza. Ahsante sana."
}