GET /api/v0.1/hansard/entries/638731/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 638731,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/638731/?format=api",
"text_counter": 566,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, namshukuru yule aliyechapisha Mswada huu na kuuleta katika Bunge ili tuweze kujadiliana. Mswada huu ni muhimu sana kwa watu wa Pwani na pengine watu wa Nyanza kwa sababu wao pia wana Ziwa Victoria. Bw. Spika wa Muda, Mswada huu unazingatia zaidi uvuvi na kuangalia hali ya samaki itakayoleta faida katika nchi yetu. Kwanza, tunashukuru kwa sababu kwa miaka mingi, watu wa Pwani wametegemea uvuvi ili kuishi. Uvuvi ni kama chakula kwa watu wa Pwani. Sisi huwa tunapata chakula kutokana na uvuvi. Pia, tunafurahia tunapoangalia bahari na kuona kweli hatukumuomba Mwenyezi Mungu tuzaliwe Pwani. Hata hivyo, kwa sababu tumezaliwa huko, ni haki yetu kuona Pwani imefaidi watu wanaotoka maeneo hayo."
}