GET /api/v0.1/hansard/entries/638733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 638733,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/638733/?format=api",
"text_counter": 568,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tuko na msemo kule kwetu unaosema: “Wavuvi wa pweza hukutana mwambani.” Maana ya msemo huu ni kwamba hata tukifanya nini sisi ni watu wa pwani, tutakutana mwambani tujue faida za uvuvi wa pweza. Mswada huu unapendekeza kuundwa kwa shirika ambalo litahakikisha kuwa wavuvi wanapata faida. Kwanza, tunajua kwamba vitu kama ngozi ya samaki wale wakubwa vina manufaa. Samaki kama papa na nguru pia wana faida yao kwa sababu nyama yao ikiuzwa, mvuvi anafaidika. Ulimwenguni kuna utalii wa aina tofauti. Kuna utalii wa kwenda baharini na hata wa mbuga za wanyama. Utalii unaofanyika Pwani ni wa baharini ambapo kuna mashindano ya boti, uvuvi wa samaki, kukukimbizana kwa bodi na kadhalika. Kwa hivyo, tunaitaka Serikali, inapozingatia usimamizi wa maswala ya uvuvi, iangalie pia swala la ongezeko kwa michezo ya baharini ambayo itasaidia watu wa pwani. Ipo hatari pia ambapo meli kubwa za kimataifa zinatia nanga katika Bahari ya Hindi. Serikali nayo haijazingatia jinsi inavyoweza kutetea mvuvi wa hali ya chini ambaye anavua na kuuza samaki ili apate faida kama mchuuzi. Kwa hivyo, kuna maswala mengi ambayo Serikali inatakikana kufikiria iwapo Mswada huu utakuwa sheria. Bw. Spika wa Muda, mambo ya kuweka samaki wanaopendeza macho inayoitwa kwa lugha ya kimombo fish aquarium, kunao mashirika mengi ambayo tunahitaji katika sheria kama hii, wale samaki ambao wanawekwa katika nyumba, wengine wanawekwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}