GET /api/v0.1/hansard/entries/638736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 638736,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/638736/?format=api",
    "text_counter": 571,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "katika mahoteli makubwa, ukienda katika viwanja vya ndege, ukienda katika maofisi ya watu binafsi, tunasema ya kwamba samaki kama wale ambao wanapatikana kule pwani, jambo la kwanza ni lazima Serikali izingatie ili ione ya kwamba samaki kama hawa wakipatikana wanaleta faida. Hasa tukiangalia ya kwamba kule Pwanindiko wale samaki wa aquarium . Tunasema kwamba Serikali iangalie na kuona ya kwamba watu wa Pwaniwanafaidika kwa uvuvi. Bw. Spika wa Muda, jambo la kusikitisha pia, tunasema ya kwamba ijapokuwa huu Mswada ambao tunategemea ya kwamba utaweza kusaidia, hasa hususan watu wa maeneo yale wanaotoka katika uvuvi wa samaki, tunasema ya kwamba, ni katika yale maeneo yaliyo na stakabadhi tofauti ama Serikali inakuwa na vitengo mbalimbali. Tunaona ya kwamba, sisi tuko na vijana wadogo ambao wako katika umri wa kuajiriwa. Ukiajiriwa katika Kenya Navy inamaana kwamba, wewe unaweza kuogelea baharini. Kuna vijana wadogo sana ambao wanavuka Fort Jesus wakienda ng’ambo ile nyingine ya English Channel na kurudi. Hao wamejua kuogelea kutoka zamani lakini tunaona ya kwamba wakienda kwa mahojiano, wao wananyimwa nafasi za kufanya kazi na watu wengine kutoka maeneof mengine wanaajiliwa. Bw. Spika wa Muda, wasichana na wavuluna wa kutoka maeneo yetu na walio na tajiriba ya kuogelea kuliko watu wa maeneo mengine hunyimwa nafasi za kazi. Ni maombi yetu watu wa Pwani wapewe nafasi ya kufanya kazi katika jeshi letu la wanamaji. Bw. Spika wa Muda, tuna Shirika la Uvuvi mashuhuri kwa jina Maritime Authority. Pia tuna shirika la kuangalia mambo ya uvuvi linalojulikana kama Fisheries Authority, na Kenya Ports Authority (KPA). Kwa miaka mingi mashirika haya yamekuwa yakisimamiwa na wakurugenzi wa kutoka nje ya maeneo ya pwani. Bodi za mashirika haya ni lazima zijumuishe watu wa kutoka makabila yote ya hapa nchini na wala si kutoka kwa kabila mbili tu. Nafasi hizo zipewe, hasa katika maeneo yale mashirika kama hayo yanapatikana. Hakuna mtu wa Pwani ambaye yuko katika nafasi ya uongozi katika KPA, isipokuwa msichana mmoja aliyepewa wadhifa wa kushikilia tu. Hatujui kama atapewa kazi hiyo lakini tunatumai kuwa nafasi hiyo itapatikana. Vile vile watu wa Pwani wanafaa kupewa nafasi za kazi katika mashirika kama Kenya Maritime Authority (KMA), Kenya Fisheries Authority (KFA) na Kenya Navy. Bw. Spika wa Muda, kuna ubepari unaoendelea hivi sasa. Mswada huu unahakikisha kwamba, kulingana na sheria, ni lazima watu ambao wanajenga nyumba zao karibu na bahari watenge nafasi ya wavuvi kwenda baharini kuvua samaki. Katika maeneo ya Malindi, Kilifi na Lamu, wavuvi hawaishi maeneo ya baharini, lakini wakitaka kwenda baharini, utaona kuta zikijengwa na ilani kutolewa kuwa sehemu ile ni mali ya mtu binafsi. Kwa hivyo, wavuvi hawawezi kufikia ufuo wa bahari ama kufanya uvuvi na kupata samaki wa kuuza, ili waweze kuwasomesha watoto wao. Kwa hivyo, Mswada huu utahakikisha kwamba wakenya hawatakosa nafasi ya kwenda kustarehe baharini ama kufanya uvuvi, ili wapate pesa na kujiendelesha katika maisha yao. Bw. Spika wa Muda, nikimalizia, sisi tunaotoka katika maeneo ya Pwani, tunajua ya kwamba Mswada huu utaweza kutetea haki zetu. Jambo kama hili linaweza kuleta The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes"
}