GET /api/v0.1/hansard/entries/638987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 638987,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/638987/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukrani Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, natoa pongezi kwa Kiongozi wa Walio Wengi kwa kutuletea Mswada huu ambao haugusii jinsia moja tu. Kwa sasa, inaweza kuonekana kana kwamba tunatetea haki ya wanawake pekee. Lakini, tutakuwa tunajitayarisha kwa wakati wowote ikiwa itatokea kuwe na upungufu katika jinsia ya kiume katika mabunge yajayo. Hivyo, watakuwa na sheria inayoweza kuwasimamia na kutoa haki katika nyanja mbali mbali katika maeneo tofauti tofauti yanayosimamiwa na mambo yanayotokana na kuchaguliwa. Mswada huu umekuja kwa wakati unaofaa. Hii ni kwa sababu tusipoupitisha, tutakuwa tumeenda kinyume na Katiba yetu. Hii inaweza kutuletea matatizo. Bunge hili linaweza kusimamishwa kwa kuhalifu Katiba tuliyoitetea kwa pamoja. Pili, katika kutetea Mswada huu, itaonyesha wananchi wetu hususani akina mama ambao hujitokeza kwa wingi kutupigia kura kwamba tunawatambua kwa jitihada walizonazo nyanjani wanapotutafutia kura na kutupitisha ili tuwawakilishe katika Bunge hili na lile la Seneti. Kwa hali ya Mswada huu, ni wazi kwamba kuna walio na akili potofu kwamba sisi tunajaribu kufungulia akina mama mlango ili watawale waume. Hivyo sivyo. Inatakikana kila mmoja aelewe kila upande wa jinsia una haki ya kutawala, kutawalwa na kusimamia katika ngazi yoyote. Tunapoupitisha huu Mswada kwa pamoja, hatutakuwa tunafungua mlango kwa wanawake pekee bali kwa jinsia zote. Mswada huu umekuja kwa wakati ufaao kuonyesha imani yetu kwa wenzetu wanaume walio katika Bunge hili. Akina mama tuliochaguliwa katika hili Bunge tumesimama na wenzetu Waheshimiwa wa kiume kupitisha mijadala tofauti tofauti. Safari hii, tunaomba mregeshe mkono ili msimame nasi katika vita hivi vya kutetea haki ya akina mama. Si haki ya akina mama tu. Inatakikana ifahamike ya kwamba palipo na mama, hata kama ni ndani ya nyumba inayotelekea, mama husimama na nyumba ikawa imara. Msimame nasi tuokoe taifa letu kutokana na kutokuwa na usawa wa kijinsia. Sitakuwa na marefu kwa sababu ya hali yangu. Ningetaka nimkosoe dadangu Mheshimiwa Wanga. Tumetoka katika yale mambo ya kutoa tu. Nipe nikupe ndio mtindo wa kisasa."
}