GET /api/v0.1/hansard/entries/639961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 639961,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/639961/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Vilevile, tungepanua zaidi mbali na kuangalia Serikali ya kitaifa kusimamia mtaalamu mmoja kwa mwaka katika kila kaunti. Serikali za kaunti kulingana na kima zinazopata, zingesimamia mwingine kwa sababu wataalam wa saratani ni wataalam aina tofauti wanaohitajika. Hata katika mfuko wetu wa Hazina ya Eneo Bunge, tungeweza kusimamia mtaalamu wa tatu hivyo tungekuwa tunapata watu watatu katika kila kaunti ambao wana utaalamu wa kutosha wa kufanya utafiti wa mapema wa hizi saratani na kuanzisha matibabu ya mapema. Ningesisitiza kuwa vituo vyetu vya utafiti na vyuo vyetu vinavyotoa mafunzo haya vinafaa kuzingatia somo hili la reflexology. Somo la reflexology hutumika kutibu saratani. Mwanzo inaweza kutibika pasi na kutumia dawa yoyote. Vilevile, saratani inaweza kusimamishwa katika ngazi ambayo imefika tukitumia njia ya reflexology . Inaweza kusimamishwa palepale hadi panapopatikana matibabu. Ningeuliza vyuo viweze kufanya utafiti huo na kujumuisha somo hilo katika vyuo vya matibabu. Ninaunga mkono. Asante."
}