GET /api/v0.1/hansard/entries/640019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 640019,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640019/?format=api",
"text_counter": 160,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Rai",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaomba kuchukua nafasi hii kukushukuru na kumshukuru aliyeleta Hoja hii. Ni wakati mwafaka kwa sababu baada ya miaka 50 tangu tupate Uhuru, itakuwa ni jambo bora kama tungeanza kuangazia masuala ya afya kuwa muhimu sana katika maisha ya jamii. Kadri tunavyoendelea kumuunga mkono Mhe. Wanga kwa sababu ya Hoja hii, lingekuwa pia wazo bora kama pengine baada ya haya yote ya kuwatuma wataalam kwenda kusomea na kuja kuleta mwelekeo bora, ingekuwa bora kujua baadhi ya wataalam fulani kielimu ili kuhakikisha kwamba masuala ya elimu katika jamii yameaangaziwa. Hii ni kwa sababu punde saratani inapomkumba mwanadamu, huwa maisha yamekwisha. Nimewahi kumpoteza mzazi wangu kutokana na saratani na rafiki yangu moja wa karibu aliyekuwa akiitwa Prof. Juma Lugogo. Ninakumbuka kabla Prof. Lugogo kuondoka duniani, aliinita hospitalini na kuniambia:- “Nimepigana na matatizo ya saratani kwa muda wa mwaka moja na nusu na hivi sasa nimefika kiwango ninainua mikono kwa sababu ninajua kwamba mambo yameshindikana na inalazimika niondoke duniani.” Alisema kitu ambacho kinaniumiza mpaka sasa kwamba: “Mimi ninaondoka na niliweza kuhimili kupigana vita hivi vya saratani kwa muda wa mwaka mmoja na nusu. Je, mtu yule wa kawaida ambaye yuko kule mashambani ataweza kuishi muda ambao nimeishi kwa sababu mimi nilikuwa ninajiweza na ninaweza kufanya mambo fulani yanayoniwezesha kuishi na kupata matibabu yanayotarajiwa?” Hili ni suala nyeti kwa sababu zamani ugonjwa wa kifua kikuu zamani kilikuwa kikitisha watu. Sasa kifua kikuu kinaweza kupata tiba hospitali fulani na hatimaye ukarejeshwa nyumbani ili uendelee kupewa dawa ukiwa huko. Saratani imefika kiwango ambacho kinachukua watu wiki baada ya wiki lakini miaka 15 ijayo huenda tukawa tulikuwa tunamsubiri Yesu Kristo kuja duniani kumbe saratani ndiyo itakuwa kiama cha mwanadamu kupoteza ama kuangamiza maisha yake katika ulimwengu huu. Unapoambiwa kuwa saratani imepatikana katika mwili wako, mara nyingi kinachokuja ni kwamba umebakisha kama miezi minne ama sita kuondoka duniani. Sisi kama viongozi ama kama watu tuliopewa majukumu, na hasa zaidi kwa sababu ya utafiti ambao umefanywa na Mhe.Wanga, nina imani kwamba takrimu hizi ambazo zimewekwa wazi kwetu--- Iko haja baada The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}