GET /api/v0.1/hansard/entries/640020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 640020,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640020/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Rai",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": "ya kupitisha Hoja hii, kuifuatilia kwa karibu sana ili kuona kwamba matokeo yake yamesaidia jamii ya Wakenya na kuleta afueni katika maisha ya mwanadamu. Kimekuwa kitu cha kawaida, pengine tumwuulize Mhe. Wanga ilimchukua muda gani kufikiria suala hili na hasa baada ya suala kumalizika pengine aangazie pia kufanya utafiti. Hii “saratani” ya ufisadi ataweza kuitumia tiba gani ama kuiletea Hoja gani kwa sababu pasipo sisi kupata suluhisho la kudumu--- Mara nyingi suala linaloulizwa ni kwamba wakati tunapohitaji msaada wa aina yoyote, huambiwa kwamba Serikali haina pesa. Lakini haijapata jibu la wale watu wanaopoteza pesa za Umma kwa sababu anayekula pesa nyingi mara nyingi huambiwa bondi yake ni shilingi 500,000. Mwenye kula shilingi kumi, bondi yake ni shilingi milioni mbili. Kwa hivyo, ninamwomba Mhe. Wanga arudi tena kizimbani afanye utafiti wa kutosha ili ajue kwamba hawa wafisadi atawapatia adhabu gani ili tupate kujua kwamba mwisho utakuwa nini kwa sababu masuala ya saratani kama tutayapitisha jinsi yalivyopendekezwa huenda tukapata afueni. Kwa hayo machache ama mengi, ninaunga mkono. Mungu atubariki."
}