GET /api/v0.1/hansard/entries/640037/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 640037,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640037/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ugonjwa wa saratani ni shetani kwa sababu uliuwa mama yangu. Mimi niliweza kuzunguka na yeye Kenya nzima. Hakuna mahali sikuenda na yeye. Tulikuwa na uwezo wa kumnunulia dawa lakini baadaye, pesa ziliisha kwa sababu ya huo ugonjwa. Kule mashinani, watu wengi hawana uwezo wa kuja huku Nairobi kutibiwa. Saa hizi, mtu akipatikana na huo ugonjwa, anajua ya kwamba yeye anaenda kufariki."
}