GET /api/v0.1/hansard/entries/640038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 640038,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640038/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": "Kama ingewezekana, tungekuwa na madaktari kule kwenye kaunti ambao watawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kuja Nairobi. Ukiangalia mwaka huu kuanzia Januari, wake wa magavana wa serikali za kaunti wamekuwa wakitembea kule mashinani na magari wakiwashughulikia wagonjwa wa saratani. Zile pesa ambazo serikali za kaunti zimepewa za kuwashugulikia watu hao hawangepatiwa. Pesa hizo zingebaki kwa Serikali Kuu. Serikali Kuu ingeweza kuwachagua madaktari ambao wangewashugulikia watu hao. Tungefanya hivyo kuliko kutuma hizo pesa za ugonjwa wa saratani kwa serikali za kaunti. Serikali za kaunti siku hizi zimekuwa za “wanyama” ambao hata hawajali mambo ya watu. Wanajali mifuko yao."
}