GET /api/v0.1/hansard/entries/64023/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 64023,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/64023/?format=api",
    "text_counter": 100,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, ukiangalia orodha hii, hasa yale majimbo sita ya Mkoa wa Pwani, utagundua kwamba Jimbo la Mombasa lina shule moja inayoitwa Shimo La Tewa. Kule Kwale kuna Shule ya Upili ya Kwale. Katika jimbo la Kilifi hakuna shule ya mkoa wala ya kitaifa. Jimbo la Taita Taveta vile vile halina shule ya mkoa wala ya kitaifa. Hali ni hiyo hiyo katika majimbo ya Tana River na Lamu. Serikali zilizotangulia za Rais mwanzilishi wa taifa aliyetuacha, Mzee Jomo Kenyatta, na Rais mstaafu, Daniel arap Moi; na Serikali ya sasa ya Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, zilichukua ahadi za kisiasa, kwamba tungesaidiwa ili maeneo yetu nayo yapate maendeleo. Ningependa Waziri Msaidizi atuambie ni hela ngapi zimewekwa kwenye Bajeti kuhakikisha kwamba sehemu hizo nazo zimepewa nafasi za shule za kitaifa na shule za mkoa?"
}