GET /api/v0.1/hansard/entries/64109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 64109,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/64109/?format=api",
"text_counter": 186,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kutuny",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "Bw. Naibu Spika Waziri amezungumzia masuala ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa New KCC. Ningependa afafanue mikakati na mipango ambayo ameweka ya kuhakikisha ya kwamba uteuzi huu utaangazia sehemu muhimu sana ambayo wao ndio wanatoa maziwa kwa wingi. Anayevaa kiatu ndiye anayejua mahali ambapo kinamfinya. Mara nyingi, uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hii umefanywa kwa kuzingatia misingi ya kisiasa na kikabila. Ningependa Waziri alihakikishie Bunge hili kwamba katika kufanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa New KCC hatazingatia misingi ya kisiasa na kikabila bali atateua mtu ambaye anaelewa masuala muhimu ya wakulima."
}