GET /api/v0.1/hansard/entries/641101/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 641101,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641101/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Waswahili husema: “Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.” “Lisemwalo lipo na kama halipo laja.” Tunafaa kuzingatia kilio cha Waturkana kwa Seneti hii. Kwa miaka mingi Kaunti ya Turkana imejulikana kwa watu wengi wenye ufukara na watoto wanaotembea uchi. Mpaka sasa tunaonyeshwa kwenye runinga shule ambazo hazijajengwa vizuri; wanafunzi wanasomea chini ya miti. Hata hivyo dua lilikubali kuwaangazia watu wa Turkana. Kwanza, tulipata siasa za ugatuzi na pia mafuta yalipatikana katika kaunti hiyo. Tatu, maji mengi yalipatikana kule yanayoweza kutumika kila siku na Wakenya wote 45 milioni kwa miaka 70. Kwa hivyo, Seneti hii haitakubali uzembe, ufidhuli na uporaji wa mali ya umma kutoka kwa viongozi waliochaguliwa na watu wa Turkana kama tulivyoambiwa na Seneta wa Turkana. Mambo aliyoyasema hapa kuhusu utumizi mbaya wa pesa za umma ni ya aibu kubwa. Lakini ajabu ni kwamba mambo haya hayafanyiki katika Kaunti ya Turkana tu bali pia kule Kaunti ya Migori na kwingineko. Ripoti ya matumizi ya pesa za mwaka 2013/2014 inaonyesha kuwa Ksh21 billioni zilitumika na ofisi ya gavana kwa njia isiyofaa. Pesa kiasi cha Kshs1.2 milioni zilitumika kununua kitanda cha gavana. Barabara ya lami ilijengwa kutumia mamilioni ya pesa na ikaharibika baada ya miezi mitatu. Viongozi wote wa kaunti hiyo sasa wana nyumba kubwa na mashamba makubwa, si tu katika Mji wa Migori bali katika miji mingine nchini. Je, hizo pesa zimetoka wapi? Wengi wao walikuwa fukara na hata waliniomba gari wakati wa kutafuta kura. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}