GET /api/v0.1/hansard/entries/641609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 641609,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/641609/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante, Mheshimiwa Spika. Nimesikia ombi la Mwenyekiti wa Kamati kuhusu fedha ambazo zinaombwa kimkopo. Ni muhimu kuwa ijapokuwa Bandari inaomba hizi fedha, kuwe na uangalifu mzuri. Mara nyingi, mashirika yanaomba hela ama fedha na mara nyingi yanakabidhiwa fedha hizo lakini ule utumizi wake unatia hofu. Naomba Bunge likubali kuwaongezea ule muda ambao wameomba. Kuongeza huo muda kutakuwa ni jambo la busara. Itawabidi nao wazingatie mambo mawili au matatu. Taasisi hii imetimiza yale ambayo yalitakiwa yafanywe katika mwango wa kwanza maana kuna kipindi cha kwanza. Waliomba fedha na tungependa kujua kama peza hizo zimetumiwa kama vile walivyosema. La pili, wakiongezewa muda na kuomba hizo fedha, wana uwezo wa kuzilipa? Halmashauri ya Bandari hivi juzi iliondoa mameneja wakuu wote Bandarini kwa sababu ya kutotenda kazi vizuri. Kwa hivyo, litakuwa ni jambo la busara kwa Kamati kwenda kuangalia ni lipi ambalo halikufanyika. Je, kabla hawajaondolewa walifanya kazi vizuri? Je, wametimiza malengo yao na shabaha za zile fedha walikuwa wameomba? Je, hizi fedha ambazo wanaziomba zitakuwa na malengo gani? Wanatarajiwa kufanya nini nazo? Je, wana nguvu ama uwezo wa kuzitumia kwa kipindi kilichobaki? Kwa hayo machache, naomba niunge mkono uamuzi wa kuwapa muda wa kukamilisha zoezi hilo."
}